Mwenyezi Mungu Anaapa kwa wakati wa dhuha, na uliokusudiwa ni wakati wa mchana mzima
Na kwa usiku utuliapo na viumbe na likashadidi giza lake. Mwenyezi Mungu Huapa kwa Atakacho katika viumbe vyake. Ama kiumbe, hafai kuapa kwa asiyekuwa Muumba wake. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina
Hakukuwacha Mola wako, ewe Mtume, wala Hakukuchukia kwa kuchelewesha kukuteremshiaWahyi
Na Nyumba ya Akhera ni bora kwako kuliko nyumba ya ulimwengu
Na Atakupa Mola wako, ewe Mtume, neema ya kila sampuli uridhike
Kwani Hakukupata, kabla ya hapo, kuwa ni yatima Akakukusanya na kukutunza
Na Akakupata hujui Kitabu wala Imani, Akakufundisha yale amabayo ulikuwa huyajui na akakuafikia kufanya amali bora
Na Akakupata masikini, Akakuletea riziki yako na Akakutajirisha kwa kutosheka na kusubiri
Basi yatima usimtende ubaya
Na muombaji usimkaripie, bali mlishe na umtimizie haja yake
Na ama neema ya Mola wako Aliyokuneemesha nayo izungumze