92.The Night

  1. Mwenyezi Mungu Anaapa kwa usiku unapoifinika ardhi na vilivyoko juu yake kwa giza lake
  2. Na kwa mchana unapofunuka mwangaza wake kutoka kwenye giza la usiku
  3. Na kwa kuumba mbea mbili: ya kiume na ya kike
  4. Kuwa vitendo vyenu vinatofautiana: kuna wenye kufanyia dunia na wenye kufanyia Akhera
  5. Ama mwenye kutoa kwenye mali yake, akamcha Mwenyezi Mungu katika huko kutoa
  6. akaamini «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na Imani hiyo na akaamini malipo yanayofungamana nayo
  7. Tutamuongoza na kumuafikia njia za kheri na wema na kumsahilishia mambo yake
  8. Na ama mwenye kuyafanyia ubakhili mali yake, asiwe na haja ya malipo ya Mola wake
  9. akakanusha neno la «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na neno hilo na akakanusha malipo yanayofungamana nalo
  10. Tutamnyoshea njia za mateso
  11. Wala hayatamfaa yeye mali yake aliyoyafanyia ubakhili atakapotumbukia Motoni
  12. Ni juu Yetu, kwa fadhila Zetu na busara Yetu, kueleza njia ya uongofu yenye kufikisha kwa Mwenyezi Mungu na ya upotevu
  13. Na Sisi Tuna mamlaka ya maisha ya Akhera na maisha ya ulimwenguni
  14. Ndipo nikawaonya , enyi watu, na kuwatisha moto wenye kuwaka, nao ni moto wa Jahanamu
  15. Hataingia Moto huo isipokuwa aliyekuwa mbaya sana. Mwenye kumkanusha Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie
  16. na akakataa kumwamini na kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake
  17. Na ataepushwa nao mchaji Mwenyezi Mungu sana
  18. Ambaye hutoa mali yake kwa kutaka nyongeza za kheri
  19. kutoa Kwake si kwa kulipa zema alizofanyiwa na mtu
  20. Lakini anatoa kwa kutaka uso wa Mola wake na radhi zake. Basi Mwenyezi Mungu atampa
  21. huko Peponi, malipo ya kumridhisha